>Mwanzo >Soma vitabu >Tokeni Mijini >Tokeni Mijini: Sehemu ya Tisa

Tokeni Mijini: Sehemu ya Tisa

SEHEMU YA TISA

 

Kukimbia Wakati wa Hatari Mwishoni mwa Pambano Hilo

 

Ishara ya Kuanza Kukimbia

 Huu sasa sio wakati kwa watu wa Mungu kuendelea kuyakaza mapenzi yao au kujilimbikizia hazina zao katika ulimwengu huu. Wakati hauko mbali, ambapo sisi, kama wanafunzi wale wa mwanzo [wa Yesu], tutalazimika kutafuta kimbilio letu maporini na mahali pasipo na watu. Kama vile kule kuzingirwa kwa Yerusalemu na majeshi ya Warumi ilivyokuwa ishara ya kukimbia kwa Wakristo wale wa Yudea, hivyo ndivyo, kule kujitwalia madaraka kwa upande wa taifa letu [la Marekani] kwa njia ya kutunga amri ile inayowalazimisha watu wote kuitunza sabato ya papa [Jumapili], kutakavyokuwa onyo kwetu sisi. Wakati huo ndipo saa itafika ya kuondoka katika miji mikubwa, tukijiandaa kuihama miji midogo ili kwenda mafichoni kwenye makazi yale ya upweke katika milima. Na, kwa sasa, badala ya kutafuta hapa [duniani] makazi yaliyojengwa kwa gharama kubwa, tungekuwa tunajiandaa kuhamia kwenye nchi ile iliyo bora, yaani, ile ya mbinguni. Badala ya kutumia fedha zetu kwa kujifurahisha nafsi zetu, tungekuwa tunajifunza kubana matumizi [kutumia fedha zetu kwa uangalifu sana]. ----- Testimonies, Gombo la 5, uk. 464,465. (1885)