>Mwanzo >Soma vitabu >Tokeni Mijini >Tokeni Mijini: Sehemu ya Tano

Tokeni Mijini: Sehemu ya Tano

SEHEMU YA TANO

 

Kujiandaa kwa Hatari Kubwa Itakayoletwa na Amri ya Jumapili

 

Nyakati za Taabu Ziko Mbele Yetu

 Haitupasi sisi kujiweka wenyewe mahali ambapo tutalazimishwa kuwa na uhusiano wa karibu sana na wale wasiomheshimu Mungu.... Hatari kubwa karibu sana inakuja kuhusiana na utunzaji wa Jumapili....

 Kundi la Jumapili linajiimarisha lenyewe katika madai yake ya uongo, na jambo hilo litamaanisha mateso kwa wale wanaokata shauri kuitunza Sabato ya Bwana [Jumamosi]. Yatupasa kujiweka wenyewe mahali pale tutakapoweza kuishika amri hiyo ya Sabato [Jumamosi] kwa ukamilifu wake. "Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote." Tena yatupasa kuwa waangalifu tusijiweke mahali pale itakapokuwa vigumu kwetu sisi wenyewe na watoto wetu kuitunza Sabato [Jumamosi].

 Endapo kwa maongozi yake Mungu tunaweza kujipatia mahali pa kuishi mbali na miji, basi, Bwana angependa kwamba sisi tufanye hivyo. Nyakati za taabu ziko mbele yetu. ----- Manuscript 99, 1908.

Harakisheni Kujiweka Tayari

 Uwezo waliopewa wafalme [Ma-Rais] ukifungamana na wema ni kwa sababu yule aliyeshika madaraka hayo yuko chini ya uongozi wa Mungu. Uwezo huo unapofungamana na uovu, basi, unafungamana na nguvu za Shetani, nao utafanya kazi ya kuwaangamiza wale walio mali yake Bwana. Ulimwengu wa Kiprotestanti umeisimamisha sanamu ya sabato [Jumapili] mahali pale ambapo Sabato ya Mungu [Jumamosi] ingepaswa kusimama, nao wanatembea katika nyayo za Upapa. Kwa sababu hiyo mimi nauona umuhimu kwa watu wa Mungu kuondoka mijini kwenda kwenye sehemu za upweke huko mashambani [vijijini], ambako wanaweza kulima mashamba yao na kuzalisha wenyewe mazao yao. Kwa njia hiyo wanaweza kuwalea watoto wao kuwa na tabia ya kawaida, inayoleta afya. Nauona umuhimu wa kuharakisha kuyaweka mambo yote tayari ili kuweza kukabiliana na hatari hiyo kubwa. ----- Letter 90, 1897.